KASEKENYA AITAKA TANROADS NA TECU KUHAKIKISHA BARABARA ZA RUNGWE ZINAKAMILIKA KWA WAKATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 20, 2025

KASEKENYA AITAKA TANROADS NA TECU KUHAKIKISHA BARABARA ZA RUNGWE ZINAKAMILIKA KWA WAKATI



Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoani Mbeya kushirikiana na mhandisi mshauri TECU kumsimamia mkandaradi CRBC anaejenga barabara za Mbaka-Kibanja km 20.7 na Katumba-Lupaso km 35.3 ili zikamilike kwa wakati.

Amesema hayo leo alipokagua ujenzi wa barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu km 79.4 wilayani Rungwe.

"Hakikisheni ujenzi unaendelea kwa viwango na barabara haijifungi wakati wote wa ujenzi ili shughuli za usafiri na uchukuzi zisiathirike", amesisitiza Eng. Kasekenya.

Amesisitiza ujenzi wa barabara zote mbili za Mbaka-Kibanja km 20.7 na Katumba- Lupaso km 35.3 uende sambamba ili ukamilike kwa pamoja na kuleta tija kwa wananchi.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya Eng. Sulemani Bishanga amesema tayari ujenzi wa barabara hizo umeanza na umefikia asilimia 4.6 na utatekelezwa ndani ya miezi 36.

Mbunge wa Busokelo mhe. Lutengano Mwalwiba ameishukuru Serikali kwa kasi ya ujenzi wa barabara hizo, kwa kutoa ajira na kukuza ujuzi kwa vijana wa Rungwe.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jafari Haniu amemshuku Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo na kumhakikishia mkandarasi ushirikiano wakati wote na kusisitiza kukamilika kwa barabara hizo kutachochea ukuaji wa biashara ya mazao ya biashara na chakula na hivyo kukuza uchumi wa wananchi wa Rungwe na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla.

Ujenzi wa barabara ya Mbaka-Kibanja Km 20.7 na Katumba- Lupaso Km 35.3 ni mkakati wa Serikali kuifungua Wilaya ya Rungwe kwa barabara za lami ambapo tayari sehemu ya Lupaso-Bujesi km 10, Bujesi-Mbaka km 12.6 na Kibanja-Tukuyu km 7 ujenzi wake umekamilika.



No comments:

Post a Comment