Na Mwandishi Wetu, Tabora
WIZARA ya Maliasili na Utalii kupitia Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Nyuki nchini, imetoa mafunzo maalum kwa mafundi seremala mkoani Tabora ya kutengeneza mizinga ya kisasa ya ufugaji nyuki.
Hatua hiyo inalenga kuongeza uzalishaji wa asali bora na kuimarisha kipato cha wafugaji nyuki.
Akifungua mafunzo hayo kwa mafundi seremala 30 kutoka wilaya tano za mikoa ya Tabora na Singida, Mkuu wa Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora, Semu Daudi, amesema lengo kuu ni kuwawezesha mafundi selemala kutengeneza mizinga bora itakayovutia nyuki kuingia na kukaa kwa urahisi, sambamba na kutumia malighafi zinazopatikana katika maeneo yao ili kupunguza gharama za uzalishaji.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanaendeshwa kwa wakati mmoja na mafunzo kwa vikundi vya wafugaji nyuki kutoka wilaya mbalimbali, hali itakayochochea ushirikiano kati ya mafundi selemala na wafugaji nyuki.
“Matarajio ya Wizara ni kuona muunganiko kati yenu na vikundi vya ufugaji nyuki ukiimarika, ili tupate asali bora na kwa wingi huku tukizingatia uhifadhi wa mazingira,” amesema Semu.







No comments:
Post a Comment