WIZARA YA FEDHA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU MZUMBE KUIMARISHA USIMAMIZI WA MALI ZA SERIKALI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, December 16, 2025

WIZARA YA FEDHA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU MZUMBE KUIMARISHA USIMAMIZI WA MALI ZA SERIKALI.



Kaimu Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, akifungua mafunzo ya usimamizi wa mali za umma, kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, waliohudhuria mafunzo ya usimamizi wa mali za umma, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, wakifuatilia mawasilisho kuhusu usimamizi wa mali za umma, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, katika mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mhadhili Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Paul Nsimbila, akizungumza kuhusu ziara ya kimasomo ya wanafunzi wa chuo hicho, wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, waliohudhuria mafunzo ya usimamizi wa mali za umma, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Msimamizi wa Mali za Serikali Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Neema Luanga, akiwasilisha mada kuhusu Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo, Nyaraka na Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Mali za Umma, kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, waliohudhuria mafunzo ya usimamizi wa mali za umma, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Msimamizi wa Mali za Serikali Mwandamizi Wizara ya Fedha Bw. Michael Luziga, akijibu maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, kuhusu usimamizi wa mali za umma, katika mafunzo ya usimamizi wa mali za umma, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Msimamizi wa Mali za Serikali Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bi. Jackline Mbuya, akiwasilisha mada kuhusu uhakiki wa Mali na usimamizi wa mali za Serikali, kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, waliohudhuria mafunzo ya usimamizi wa mali za umma, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, wakiuliza maswali kuhusiana na mada zilizowasilishwa katika mafunzo ya usimamizi wa mali za umma, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Meza kuu ikiongozwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, ikiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo Kikuu Mzumbe, walioshiriki katika mafunzo ya usimamizi wa mali za umma, kwa na wanafunzi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, yaliyoandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Meza kuu ikiongozwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, ikiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma masomo ya ununuzi na ugavi, yaliyoyanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)


Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.


Wizara ya Fedha, imeahidi kuendelea kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe (MU) katika nyanja mbalimbali ikiwemo kujengeana uwezo katika masuala ya ununuzi, ugavi na usimamizi wa mali za Serikali ili kuandaa wahitimu waliobobea katika sekta hizo.

Hayo yalibainishwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, wakati akifunga mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaosoma Shahada ya Ununuzi na Usimamizi wa Mali “Procurement and Assets Management”. Mafunzo yalioandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha na kufanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wanafunzi hao kuhusu masuala yanayohusu Usimamizi wa Mali za Umma ikijumuisha Uelewa kuhusu Sheria, Sera, Kanuni na miongozo ya Usimamizi wa Mali za Umma, taratibu za Uondoshaji wa Mali za Umma, taratibu za uhakiki wa Mali za umma pamoja na Daftari la Kieletroniki la Usimamizi wa Mali za Serikali (GAMIS).

‘‘Tunawapongeza Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa kuanzisha Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Mali za Serikali (Bachelor’s Degree in Government Assets Management), kwa kuwa ni hatua muhimu inayolingana na mahitaji halisi ya soko la ajira na majukumu ya Serikali,’’ alisema Bw. Mwenda.

Bw. Mwenda alisema Serikali imeendelea kuboresha mifumo ya ulipaji na usimamizi wa mali za Serikali ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hatua inayolenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma.

‘’Serikali kwa sasa imepiga hatua kubwa katika matumizi ya mifumo, ikiwemo Mfumo wa Usimamizi wa Mali za Serikali (GAMIS), Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi ya Umma (NeST) na Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) hii ni kati ya mifumo ambayo imeongeza uwazi na uwajibikaji pamoja na kuziba mianya ya rushwa’’, alifafanua Bw. Mwenda.

Alitoa rai kwa wanafunzi hao kutumia fursa hiyo ya ziara ya mafunzo kujijenga kitaaluma, kuongeza maarifa na kuendelea kubadilishana uzoefu huku wakijituma katika masomo na kufaulu kwa kiwango cha juu ili waweze kushindana katika soko la ajira

Awali, akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Chotto Sendo, alisema Wizara imeendelea kuboresha na kuimarisha mifumo ya utunzaji wa mali za umma kutokana na mabadiliko mbalimbali ya sheria ambayo yamekuwa yakitokea nchini.

‘’Mwaka 2009 Serikali iliiunda Idara ya usimamizi wa mali za Serikali kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya usimamizi wa mali za umma nchini. Katika kutekeleza majukumu hayo mwaka 2012 Wizara ilitoa Mwongozo wa Usimamizi wa Mali za Umma, 2012 ambao ulihuishwa mwaka 2019 (PAMG R.E, 2019) alifafanua Bw. Sendo.

Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Mali za Serikali (GAMIS) ambao umewezesha utunzaji mzuri wa taarifa za mali za Serikali nchini na imeendelea kuhuisha Mfumo huo (GAMIS Version II, 2025) kuendana na mahitaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitivo cha Ununuzi na Ugavi na Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Paul Nsimbila, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo alieleza kuwa yatawajengea wanafunzi uwezo na weledi kwa vitendo.

Alisema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kitaendelea kushirikiana na Wizara katika hatua ya kujengeana uwezo wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wake, kwa kutumia uzoefu wa wataalamu wa Wizara waliobobea katika usimamizi wa mali za serikali.

Dkt. Nsimbila alitoa rai kwa Wizara ya Fedha kuendeleza ushirikiano utakaojenga uzoefu kwa wanafunzi na kukiwezesha Chuo Kikuu Mzumbe kuandaa wahitimu waliobobea katika sekta ya usimamizi wa mali nchini.

Mafunzo hayo ya siku moja yaliratibiwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali yalihudhuriwa na wanafunzi 150 na Wahadhiri Saba (7) kutoka Chuo Kikuu Mzumbe-Ndaki ya Morogoro.

No comments:

Post a Comment