MNZAVA AWASIHI VIJANA KUTOJIHUSISHA NA UHALIFU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 6, 2025

MNZAVA AWASIHI VIJANA KUTOJIHUSISHA NA UHALIFU



Makundi mbalimbali ya Vijana wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kajamii ikiwemo bodaboda wametakiwa kuacha kujihusisha na matukio yenye kuharibu amani ya nchi na badala yake wawe mstari wa mbele katika kuilinda na kuitunza amani iliyopo.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la korogwe vijijini Mheshimiwa Timotheo Mnzava katika ziara yake ya kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo madereva bodaboda.

Akizungumza na vijana wa jimbo hilo amesisitiza kuwa ni vyema kuilinda amani iliyopo kwa nguvu zote huku akisistiza vijana hao kutojihusisha katika maandamano yanayotajwa kufanyika desemba 9 ambayo si halali kisheria kwani wapo baadhi ya vijana walioweza kupata athari mbalimbali ikiwemo ulemavu katika maandamano ya oktoba 29.

Kwa upande wao baadhi ya vijana hao wameahidi kutojihusisha na matukio ya ukatili badala yake watakuwa mabalozi wazuri wa amani.

No comments:

Post a Comment