Oryx Gas Yaongeza Muda wa Kampeni ya Gesi Yente Hadi Desemba 15 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 1, 2025

Oryx Gas Yaongeza Muda wa Kampeni ya Gesi Yente Hadi Desemba 15

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imekabidhi zawadi mbalimbali kwa wateja walioshinda kupitia kampeni yao ya GESI YENTE, ambayo inalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Akizungumza Desemba 1, 2025 wakati wa hafla ya utoaji zawadi, Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Shaban Fundi, alisema Oryx itaendelea kuwekeza katika miundombinu na kupanua mtandao wa usambazaji ili kusaidia utekelezaji wa ajenda ya matumizi ya nishati safi kwa afya bora, uhifadhi wa mazingira na maendeleo endelevu.

“Kama Tanzania imeweka lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, sisi kama Oryx hatuko nyuma. Tumejipanga kuhakikisha huduma zetu zinawafikia wananchi kupitia mawakala wakubwa na wadogo,” alisema Fundi.

Aidha, alisema zaidi ya wateja milioni moja wameshiriki kampeni hiyo kwa kutuma ujumbe kupitia kadi zilizowekwa katika mitungi ya gesi ya Oryx, hatua inayodhihirisha imani ya wateja katika ubora wa bidhaa na huduma zao.

Fundi alitoa tahadhari kwa wananchi dhidi ya mawakala wasiowaaminifu wanaobadilisha mitungi ya Oryx na kuwaonya wateja kuhakikisha wanabaki na mitungi yao halali.

“Ukishautoa mtungi wako wa Oryx si rahisi kuupata tena. Ni muhimu kuhakikisha mtungi wako unabaki mikononi mwako,” alisisitiza.

Kampeni yaongezewa muda

Kuhusu kampeni ya GESI YENTE, alisema ilianza Agosti 13, 2025 na ilipangwa kudumu kwa miezi mitatu. Hata hivyo, kutokana na mwitikio mkubwa na maombi ya mawakala, muda umeongezwa hadi Desemba 15, 2025.

“Tangu uzinduzi, tumefikia wateja wengi na tumeshuhudia jumbe nyingi kupitia kadi zilizopo kwenye mitungi yetu. Zaidi ya watu milioni moja wameshiriki, ndiyo maana tumeongeza muda,” alisema.

Washindi wapongeza kampeni

Baadhi ya washindi wa zawadi mbalimbali ikiwemo majiko ya gesi, baiskeli, pikipiki na mabegi ya shule walipongeza Oryx Gas kwa ubunifu wa kampeni inayochochea matumizi ya nishati safi na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.

Irene Godfrey, mkazi wa Mbezi Beach aliyejinyakulia pikipiki, alisema ushindi huo umempa mtaji kwa kuwa atautumia usafiri huo kwenye shughuli za uzalishaji.

“Gesi ya kupikia ni mkombozi wa afya na mazingira. Nashukuru Oryx kwa kampeni hii,” alisema Irene.

Naye Elikana Madirisha, aliyeshinda jiko la Oryx, alisema zawadi hiyo itarahisisha maandalizi ya chakula na kupunguza muda wa kukaa jikoni.










No comments:

Post a Comment