
Na. Jeremiah Mbwambo, Singida
Kambi hiyo inafanyika kwa ushirikiano wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa mafunzo na huduma mkoba na Mkuu wa msafara Bw. Rayhan Mbisso ameeleza kuwa kambi hii imekuja na madaktari bingwa wa moyo kwa watoto na watu wazima
"Tumekuja na madaktari bingwa wa moyo kwa watu wazima na watoto, hii inatoa fursa kubwa kwa Wananchi wa mkoa wa singida kufanya uchunguzi na kupata matibabu ya Moyo kwa watoto kwa siku tano mfululizo kuanzia leo"amesema Bw. Mbisso
Kaimu Mganga mfawidhi Dkt. David Mwasota amewapokea madaktari Bingwa na Wataalamu wa matibabu ya moyo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa
"Tumetangaza ujio wenu na mwitikio wa siku ya kwanza ni mkubwa wanawasubiri muweze kuwapa huduma, nimatumaini yetu siku zinavyo endelea tutakuwa na wagonjwa wengi zaidi ya siku ya leo"amesema Dkt. Mwasota
Hospitali ya Benjamin Mkapa imetoa madaktari na wataalamu wa mayo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma katika maeneo yanayo izunguka Hospitali hiyo na huku ikiendelea kuadhimisha miaka kumi ya utoaji huduma zake tangia ilipo anzishwa





No comments:
Post a Comment