WATUMISHI WA GPSA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA TSH 325.13 MILIONI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 21, 2026

WATUMISHI WA GPSA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA TSH 325.13 MILIONI


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro, imewafikisha mahakamani watu wanne wanaodaiwa kuhusika na makosa ya kuongoza genge la uhalifu wa wizi na utakatishaji fedha zenye thamani ya Shilingi 325,130,000, zilizotokana na wizi wa mafuta ya petroli na dizeli kutoka kwa Wakala wa Ununuzi wa Serikali (GPSA).

Watuhumiwa hao ni BENJAMIN MKAPA NYAKUNGA, BENSON MWAMKUNGA, HARUNA MUSSA MUYANGO na RASHIDI MOHAMED KINDINDINDI, ambao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Novemba 20, 2026, na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi namba 26623/2026.

Kesi hiyo ilisomwa na Mawakili wa Serikali kutoka TAKUKURU, Brian Mzava na Fuja Ngalo, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa, Mhe. Janeth Kanyage.

Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu wa wizi pamoja na utakatishaji fedha zinazodaiwa kutokana na wizi wa mafuta ya petroli na dizeli kutoka GPSA.

Baada ya kusomewa mashtaka, watuhumiwa walipelekwa mahabusu kwa kuwa makosa yanayowakabili hayana dhamana.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Desemba 3, 2026.

No comments:

Post a Comment