TANZANIA NI MFANO WA AMANI NA MSHIKAMANO DUNIANI- GUTERRES - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, December 14, 2025

TANZANIA NI MFANO WA AMANI NA MSHIKAMANO DUNIANI- GUTERRES


Ujumbe wa Mheshimiwa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 14 Desemba 2025, wakati akipokea Ujumbe Maalum kutoka Tanzania.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Antonio Guterres, amesema kuwa “Tanzania imekuwa ni rejea muhimu ya amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote,” wakati akipokea Ujumbe Maalum kutoka Tanzania.

Ameeleza kuwa taswira ya Tanzania kama kielelezo cha amani ilijaribiwa katika uchaguzi wa hivi karibuni uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, lakini taifa liliweza kuvuka mtihani huo kwa mafanikio, ikiwa ni mara ya kwanza kukabiliwa na changamoto hiyo.

“Umoja wa Mataifa ungependa kuona Tanzania inaendelea kubaki katika umoja wake na kuwa mfano bora kwa mataifa mengine,” alisema Katibu Mkuu Guterres alipokuwa akipokea Ujumbe Maalum uliobeba salamu na ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Kombo, pamoja na ujumbe wake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa yenye maana, jumuishi na shirikishi ili kushughulikia chanzo cha matukio ya vurugu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba, pamoja na kutafuta njia za kudumu za kuyazuia yasijirudie tena.


Aidha, aliahidi msaada kamili wa Umoja wa Mataifa wakati wote na hata baada ya Tume ya Uchunguzi iliyoanzishwa nchini Tanzania kukamilisha majukumu yake.

No comments:

Post a Comment