TRA YATOA SOMO LA UWAZI NA UWAJIBIKAJI, YABEBA TUZO MBILI ZA NBAA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, December 5, 2025

TRA YATOA SOMO LA UWAZI NA UWAJIBIKAJI, YABEBA TUZO MBILI ZA NBAA



MAMLAKA ya Mapato tanzania (TRA), imeibuka Mshindi wa kwanza wa jumla katika tuzo ya Uandaaji wa Hesabu za Kifedha zinazozingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS), zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Pia imeibuka mshindi wa kwanza katika tuzo ya kipengele cha Taasisi za Serikali (Government Agency Categories).

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Naibu Waziri wa Fedha Laurent Luswetula, alizipongeza taasisi zilizoibuka na ushindi, huku akisema wizara hiyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa NBAA, ili kuendelea kuzalisha wahasibu na wakaguzi bora.

Pia alisema serikali itahakikisha NBAA inasimama imara ili iendelee kuzalisha watendaji bora kwa maslahi mapana ya taifa.

"Wizara ya fedha itaendelea kuhakikisha inatoa ushirikiano kwa NBAA ili kuzalisha wahasibu na wakaguzi bora kwa mslahi mapana ya taifa letu."alisema

Vilevile Naibu Waziri huyo alipongeza NBAA kwa kuendelea kupanua wigo wa kuongeza washiriki kila mwaka.

Naye Naibu Kamishina Mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha lisema, tuzo waliyopata ina umuhimu mkubwa, kwani inachangia kuonesha utendaji wao unakubalika Kimataifa.

Pia alisema tuzo hiyo inaonesha umahiri na ubunifu uliyopo kwa watumishi wa mamlaka hiyo.

"Tuzo hii ina umuhimu sana kwetu, inachangia kuonesha utendaji wetu unakubalika Kimataifa na ina waonesha Walipa Kodi kwamba kila shilingi inayokusanywa inafika katika mfuko Mkuu wa Serikali."alisema

Vilevile Mcha aliwashukuru Walipa Kodi kwa kuendelea kulipa kwasababu TRA imeendelea kuvuka malengo ya ukusanyaji mapato kila mwaka.

Kwamujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Profesa Slyivia Temu, katika hafla hiyo jumla ya taasisi 86 za Umma na binafsi zimeshiriki katika kujipima ubora wa kuwasilisha taarifa za fedha kwa mwaka 2024.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Pius Maneno, lengo la tuzo hizo ni kuhakikisha taarifa za hesabu zinazotolewa zinakuwa na uwazi na uwajibikaji.

Alifafanua kuwa, tuzo hizo ni taarifa za hesabu za kuanzia Januari mwaka 2024 hadi Desemba, ambazo zimezalishwa kwa kufuata hesabu za Kimataifa na zilizopata hati safi.

No comments:

Post a Comment