Akizungumza Disemba 1, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha wadau wa mpango wa chakula shuleni, Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji Sera za Elimu Msingi, Victor Bwindiki, alisema kikao hicho kinalenga kubadilishana uzoefu, kujadili mafanikio na changamoto pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha utoaji wa chakula mashuleni.
“Kila mshiriki atapata nafasi kueleza mbinu bora, masomo tuliyojifunza na changamoto zinazojitokeza. Tutajadili kwa pamoja namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kuboresha mpango wa chakula shuleni nchini,” alisema Bwindiki.
Kwa upande wake, Vera Kwara, Mkuu wa Kitengo cha Lishe, VVU na Mipango ya Shuleni kutoka WFP, aliwashukuru wadau kwa juhudi zao katika kuimarisha mpango huo muhimu kwa mustakabali wa elimu nchini.
“Kwa baadhi ya watoto, mlo wa shule ndio chakula chenye lishe kamili wanachokipata kwa siku. Hivyo kuongeza utofauti wa vyakula, hususan vyenye protini na virutubisho, ni hatua muhimu,” alisema.







No comments:
Post a Comment