KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU, UTAMADUNI NA MICHEZO YAPONGEZA MABORESHO YA SERA NA MITAALA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 23, 2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU, UTAMADUNI NA MICHEZO YAPONGEZA MABORESHO YA SERA NA MITAALA


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza mageuzi makubwa yaliyofanywa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo la 2023) pamoja na Mitaala iliyoboreshwa, ikielezwa kuwa hatua hiyo italeta mabadiliko makubwa katika ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Pongezi hizo zimetolewa Januari 22, 2026 jijini Dodoma, katika kikao kilicholenga kutoa elimu kwa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa sera na mitaala mipya. Wajumbe wamesisitiza kuwa mageuzi hayo ni ya kimkakati na wameishauri Serikali kuongeza uwekezaji katika Mkondo wa Amali, unaotoa mafunzo ya ujuzi katika fani mbalimbali ili kuongeza ajira na umahiri wa wahitimu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ameeleza kuwa serikali kupitia wizara husika inaendelea kutekeleza sera na mitaala hiyo kwa lengo la kuandaa wahitimu wenye ujuzi na umahiri.

Aidha, amebainisha kuwa tayari shule za sekondari 103 za amali zimejengwa nchini kote na shule za ufundi zilizokuwepo zimeimarishwa, hatua inayoongeza fursa za mafunzo ya vitendo kwa vijana.



No comments:

Post a Comment