KAMATI YA MIUNDOMBINU YAPOKEA TAARIFA ZA TAASISI ZA WIZARA YA UJENZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 22, 2026

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAPOKEA TAARIFA ZA TAASISI ZA WIZARA YA UJENZI



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepokea na kujadili taarifa ya muundo na majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi za Wakala wa Barabara (TANROADS), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) iliyowasilishwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega leo tarehe 22 Januari, 2026.

Katika wasilisho lake, Waziri Ulega, ameshukuru na kutoa pongezi kwa Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha ili kutekeleza miradi ya ujenzi nchini ambayo imesaidia kuleta maendeleo na kufungua fursa za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Waziri Ulega ameahidi kushirikiana na kamati hiyo na kuzingatia maoni wanayoyatoa ili kuboresha utendaji, kuongeza uwajibikaji na kuhakikisha thamani ya fedha za umma zinalindwa.










No comments:

Post a Comment