Kanisa la Mlima wa Moto laja na kongamano la Anza mwaka na Bwana - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, January 25, 2026

Kanisa la Mlima wa Moto laja na kongamano la Anza mwaka na Bwana

Na Mwandishi Wetu

KANISA la Mlima wa Moto la Mikocheni jijini Dar es Salaam, limezindua kongamano la kuombea nchi amani lijulikanalo kama Anza mwaka na Bwana na miongoni mwa yatakayozungumziwa ni ujasiriamali.

Akizungumza leo Kanisani hapo, Askofu wa Kanisa hilo, Rose Mgeta alisema miongoni mwa yatakayofanyika kwenye kongamano hilo la siku nane ni kuombea nchi amani ili isirudi kwenye machafuko ya Oktoba 229 mwaka jana.

Alisema kwenye kongamano hilo vijana pia watafundishwa masuala ya ujasiriamali na biashara ili waweze kutambua fursa na kuzitumia kuondokana na umaskini.

Alisema vijana watakaohudhuria kongamano hilo mbali na neno la Mungu watafundishwa mbinu mbalimbali za kufafuta fedha kama ujasiriamali na namna ya kutumia fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo.

Askofu Mgetta alisema maadili kwa sasa yanakwenda kombo hivyo kwenye kongamano hilo watafundisha pia vijana kuzingatia maadili ikiwemo kuheshimu wazazi na watu wanaowazunguka.

“Vijana waishi maisha ya heshima kwa wazazi na watu wanaowazunguka ili wapate heri duniani, kuheshimu wazazi ni Baraka kwa hiyo tutawakumbusha vijana umuhimu wa kuwakumbuka na kuwasaidia vijana,” alisema

Akitoa shukrani zake kwa kufanikiwa kupata ubunge, Mbunge wa Mlimba (CCM), Dk Hellen-Rose Rwakatare aliwataka waumini hao kuomba na kujituma ili waweze kufanikiwa.

“Maandiko matakatifu yanasema usiposhukuru kwa kidogo hutapewa hata hicho kikubwa, nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuibuka na ushindi mkubwa kuanzia kwenye kura za maoni hadi Uchaguzi Mkuu, mnafahamu Mungu amenitendea mengi sana ndani ya miaka miwili,” alisema

“Tulianza mchakato pamoja hapa, tuliomba tukapita kura za maoni, nikaja kuomba tena, nikaenda kwenye uchaguzi mkuu, mungu akanisaidia tena, nilishinda kwa kura nyingi sana kwenye lile jimbo haijawahi kutokea, nilishinda kwa asilimia 95.9,’ alisema

“Namshukuru sana Askofu Rose Mgeta, Askofu Dunstan Maboya kama mnakumbuka aliniombea akaniwekea mikono kichwani akasema Baraka za mama ziko juu yangu, kwa hiyo nawashauri muishi kwa kutenda mema kwasababu mema yataambana na nyinyi,” alisema

“Mama yangu alipanda mbegu, alitenda mema sana kiasi kwamba sisi watoto wake kila tunakopita tunafunguliwa milango, kama unanafasi ya kutenda jema tenda usingoje shukrani hata adui yako mtendee mema, msikimbie kimbie kubadilisha makanisa ombeni mkiwa hapahapa Mungu ni huyu huyu,” alisema

“Ombeni kwa kufuata fomyula msiombe mkiwa mmekaa tu bila kufanyakazi, lile ombi unaloomba simama ukalifanyie kazi, mfano unaomba kazi unakaa nyumbani, hiyo kazi itakukuta nyumbani? Unaomba kuongezewa cheo lakini hufanyi kazi kwa bidii cheo huwezi kupata,” alisema

“Msichana unaomba upate mchumba basi jitahidi upendeze, na mvulana unataka mchumba basi jitahidi uwe na tabia njema ili uweze kujibiwa ombi lako usika kae tu,’ alisema.

“Mungu anasema nitabariki kazi ya mikono yako lakini huwezi kubarikiwa ukiwa umekaa nyumbani, lazima msimame mfanye kazi kwa bidii kwa hiyo lazima msimame kwa dhati na msimame kwa nguvu kuomba” alisema

“Mama yangu hakuwa anapenda umaskini na wengi humu mmeombewa hapa hapa na mmeondokana na umaskini kwa hiyo mnaona hakuna lisilowezekana chini ya madhabahu huu,” alisema

No comments:

Post a Comment