MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA YAANZA RASMI JIJINI TANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 19, 2026

MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA YAANZA RASMI JIJINI TANGA


Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema (Katikati), akizungumza kwenye Maarifa FM na wananchi wa Jiji la Tanga, kuhusu Maadhimisho ya Tano ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.

Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema (Katikati), Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania kanda ya kaskazini (TIRA), Dkt. Emmanuel Lupilya (upande wa kulia) Meneja Msaidizi wa Idara ya Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Noves Moses (upande wa kushoto) wakiwa Maarifa FM wakizungumza na wananchi wa Jiji la Tanga, kuhusu Maadhimisho ya Tano ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.

Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Usagara walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yatakayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.

Baadhi ya wananchi wakipatiwa elimu ya fedha na Wataalam kutoka Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Tano ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi", yatakayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga. Maadhimisho hayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Tanga)


Na Eva Ngowi na Chedaiwe Msuya, WF, Tanga


Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwa mwaka 2026 yameanza rasmi leo tarehe 19 Januari, 2026 katika Viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya fedha, ikiwemo matumizi sahihi ya huduma za kifedha, umuhimu wa kujiunga na mifumo rasmi ya fedha pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiuchumi kwa maendeleo endelevu.

Akizungumza katika kituo cha Rafio cha Maarifa FM, Jijini Tanga, Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema, amesema maadhimisho hayo yanashirikisha taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo benki, kampuni za bima, taasisi za mikopo pamoja na wadau wengine wa huduma za fedha, ambao wanatoa elimu, ushauri na huduma moja kwa moja kwa wananchi.

Bi. Mjema alizungumza akiwa ameambatana na Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Kaskazini, Dkt. Emmanuel Lupilya, pamoja na Meneja Msaidizi wa Idara ya Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Noves Moses.

Kwa upande wake, Dkt. Emmanuel Lupilya amesema maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kupata elimu kuhusu umuhimu wa bima, haki na wajibu wa mteja wa bima pamoja na namna ya kuchagua huduma sahihi za bima kulingana na mahitaji yao, jambo litakalosaidia kupunguza athari za majanga na hasara za kifedha.

Naye Meneja Msaidizi wa Idara ya Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Noves Moses, ameeleza kuwa BoT inatumia maadhimisho hayo kutoa elimu kuhusu sera za fedha, usalama wa matumizi ya mifumo ya malipo ya kielektroniki pamoja na tahadhari dhidi ya udanganyifu wa kifedha, ili kuongeza uaminifu wa wananchi katika matumizi ya huduma za kifedha.

Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi,” na ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kujenga jamii yenye uelewa wa masuala ya fedha, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na kuinua maisha ya wananchi kwa ujumla.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa 2026 yanatarajiwa kuvutia wananchi wengi kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Tanga, yakitoa fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kupata huduma muhimu za kifedha kwa urahisi katika eneo moja.

No comments:

Post a Comment