
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa na Timu ya Uratibu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kutoka Wizara ya Fedha katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jiji la Tanga kuhusu maadhimisho ya tano ya ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu

Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jiji la Tanga kuhusu maadhimisho ya tano ya ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu

Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema akimpokea Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maadhimisho ya tano ya ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.

Baadhi ya picha za Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ikiwa maadhimisho ya tano ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yanayoendelea katika Viwanja vya Usagara, Jijini Tanga, ambayo yatazikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hitadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Tanga na mikoa ya karibu.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Tanga)
Na Eva Ngowi na Chedaiwe Msuya, WF, Tanga
Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema, pamoja na timu ya uratibu, wamefanya majadiliano na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba, kujadili kuhusu Maadhimisho ya Tano ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyoanza jana na yatazinduliwa rasmi kesho katika viwanja vya Usagara Jijini Tanga.
Majadiliano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Jiji la Tanga, ambapo pande zote zilijadili kwa kina utekelezaji wa maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha chini ya kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi.” Na yanajumuisha wadau mbalimbali wa sekta ya fedha kutoka Mkoa wa Tanga na mikoa ya jirani.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Dadi Kolimba alisema kuwa mkoa unaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanikiwa na kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuwaalika wakazi wa mkoa wa Tanga kushiriki katika maadhimisho hayo ili kupata fursa na elimu ya namna ya kijikwamua kiuchumi.
Alibainisha kuwa Wiki ya Huduma za Fedha ni fursa muhimu kwa wananchi kupata elimu ya fedha, kuongeza uelewa wa huduma rasmi za kifedha na kuchochea maendeleo ya kiuchumi, hususan kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.
Kwa upande wake, Bi. Dionisia Mjema alisema kuwa lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi ya kifedha kupitia elimu ya fedha, pamoja na kuwakutanisha taasisi ndogo za fedha, benki, mifuko ya hifadhi ya jamii na wajasiriamali, ili kujenga mshikamano na kukuza ujumuishaji wa kifedha nchini.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanaendelea Jijini Tanga, yakilenga kufikisha elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali ya jamii kama njia ya kuimarisha ustawi wa kiuchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment