
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali kuhusu fursa za kuendelea kukuza uchumi wa nchi.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, aliyekuwa akitoa maelezo ya Shirika hilo, walipomtembelea ofisi kwake Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali kuhusu fursa za kuendelea kukuza uchumi wa nchi.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiongoza kikao kati yake na Uongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), ambapo walijadiliana masuala mbalimbali kuhusu fursa za kuendelea kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya bima, Treasury Square, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Mwantum Sultan, akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani) na Uongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, baada ya kukutana na kujadili masuala mbalimbali kuhusu fursa za kuendelea kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya bima, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, (wa pili kushoto), Mkugenzi wa Huduma za Sheria NIC, Bi. Asma Suleiman Mohamed (kushoto), Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Mwantum Sultan (kulia), na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichojadili masuala mbalimbali kuhusu fursa za kuendelea kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Na. Farida Ramadhani na Silya Kombe, WF, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameliagiza Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuandaa mikakati madhubuti ili kuendana na mwelekeo wa mipango ya muda mrefu ya nchi, ambayo inaonesha fursa kubwa za ukuaji wa Uchumi, hususan katika Sekta ya Bima.
Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ametoa maelekezo hayo Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu fursa za kuendelea kukuza uchumi wa nchi.
Alisema katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, kuna fursa kubwa za kiuchumi ambapo sekta ya bima inatajwa kuwa miongoni mwa sekta zenye mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo, hivyo NIC ni lazima ijipange namna ya kuchangamkia fursa hizo.
“Tuna mipango mikubwa ya nchi, tukiangalia Mpango wa Miaka Mitano na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ambayo inaonesha fursa za kiuchumi na fursa katika sekta ya bima, NIC kama Shirika la umma lazima tujipange kuelekea mipango hiyo kwasababu kutakuwa na maendeleo ya viwanda, kutakuwa na kanda za viwanda na kanda maalum za viwanda, kilimo na vitu vingine” alisema Mhe. Balozi Khamis.
Aidha, aliwaagiza kujitangaza na kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya bima kwa wananchi ili waweze kutambua fursa zinazopatikana katika sekta hiyo pamoja na umuhimu wa bima hususan wakati wa majanga.
Kwa upande wake Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, alisema Shirika hilo limekuwa likifanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake.
Alisema wamejipanga kutoa huduma bora nchini kote na kuwekeza zaidi kwenye miradi ya maendeleo kama viwanda, miundombinu na masoko ya mitaji lengo kuu likuwa ni kuongeza mapato ya Taifa.

No comments:
Post a Comment