MAKONDA KUWASILISHA UJUMBE MAALUM WA TANZANIA KWA RAIS WA CAF - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 16, 2026

MAKONDA KUWASILISHA UJUMBE MAALUM WA TANZANIA KWA RAIS WA CAF


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda amesema kuwa safari yake nchini Morocco imebeba ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenda kwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe kuhusu makabidhiano rasmi na kuthibitisha dhamira ya Tanzania kuwa moja ya nchi mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Makonda amesema hayo Januari 16, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, saa chache kabla ya kuelekea nchini Morocco kwa ziara maalumu ya kikazi.

Amesema kuwa, hatua hiyo ni matokeo ya juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha sekta ya michezo, hususan miundombinu ya viwanja, usafiri, malazi na maandalizi ya kiufundi yanayokidhi viwango vya kimataifa.

Ameongeza kuwa, Tanzania kuwa wenyeji wa AFCON 2027 utakuwa fursa adhimu kutangaza sekta utalii, kuimarisha diplomasia ya michezo, pamoja na kukuza uchumi kupitia ajira na biashara zitakazotokana na mashindano hayo.



No comments:

Post a Comment