Na Maryam Elhaj WMJJWM- Dodoma
Serikali imesema Maendeleo ya Taifa lolote inategemea Malezi na Makuzi kwa watoto ili kujenga Taifa imara lenye uzalendo upendo kwa Nchi na uchapa kazi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu wakati akifungua Kikao kazi cha Sekretarieti ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kilichofanyika Jijini Dodoma.
Dkt. Jingu amesema ni muhimu kufanya thathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto ili kujua mafaniko na changamoto ya utekelezaji wa Mpango huo ili kujua na Mpango thabiti utakaosaidia kuondoa changamoto zilizobainishwa wakati wa utekelezaji wa mpango Mpango huo.
Ameongeza kuwa kuimarisha Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ni kuweka Msingi imara kwa Taifa kwa kuzingatia Malezi Bora kwa watoto katika nyanja mbalimbali zikiwemo Afya Lishe na Elimu.
Naye Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sebastian Kitiku amesema Wizara inafanya tathmini hiyo ili kuona shabaha za utekelezaji wa Mpango huo kama zimefikiwa na changamoto zake ili kuja ma Mpango utakaojibu changamoto na kuimarisha Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa Maendeleo ya Taifa.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania (TECDEN) Mwajuma Kibwana amesema Mtandao huo utaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine ili kufanya thathimini ya Mpango huo ili kuhakikisha watoto wa Tanzania wanapata Msingi Bora wa Malezi na manufaa yao, familia, Jamii na Taifa kwa ujumla.





No comments:
Post a Comment