Ndoto Yatimia, Waziri Kijaji Ampokea Braydon Bent Tanzania - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 27, 2026

Ndoto Yatimia, Waziri Kijaji Ampokea Braydon Bent Tanzania


Ndoto ya siku nyingi ya kijana shabiki mashuhuri duniani wa klabu ya Manchester City ya Uingereza, Braydon Bent, kutembelea Tanzania leo imetimia.

Ni kama safari iliyochukua karne hivi ya kutoka tu Etihad Stdium hadi Serengeti! Shabiki huyo mtopezi wa Manchester City anasifika kwa kurekodi video akiongea Kiswahili na alipata kuahidiwa kuja Tanzania tangu mwaka 2020.

Leo, hatimaye, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi wametimiza ndoto ya shabiki huyo ambaye amepata pia kuwahoji mastaa kama Neymar, Aguero, Kocha Pep Guadiola na sasa akiwa mtangazaji wa mechi za Man City na pia akiwa na vipindi Sky News. 

“Ilikuwa ndoto yangu kubwa kufika nchi hii nzuri. Kwa mapokezi haya naona kabisa tayari safari yangu imeanza vyema kabisa,” alisema Braydon akiwa ameambatana na Bw. Mark Bent, baba yake mzazi.

Karibu kwenye nchi bora kwa Utalii wa safari duniani.

No comments:

Post a Comment