PROF. SHEMDOE ASHUKURU KWA DUA BAADA YA KUPEWA DHAMANA YA KUWATUMIKIA WANANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 2, 2026

PROF. SHEMDOE ASHUKURU KWA DUA BAADA YA KUPEWA DHAMANA YA KUWATUMIKIA WANANCHI




Na James Mwanamyoto - Lushoto


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) na Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amefanya dua maalum nyumbani kwake Lushoto pamoja na viongozi wa dini, kama ishara ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia fursa ya kuwatumikia wananchi.

Akizungumza baada ya dua hiyo, Disemba 31 2025, Prof. Shemdoe amesema ameona ni vyema kurejea mbele za Mungu kwa kutoa shukrani, kwani safari yake ya kugombea Ubunge ilianza kwa dua ya kuomba baraka na ushindi, akishirikiana na viongozi hao wa dini.

Aliongeza kuwa, mara baada ya kupata uteuzi wa kugombea Ubunge, alishirikiana na viongozi hao wa dini kumuomba Mwenyezi Mungu kuwavusha salama wakati wa kampeni na sasa wamerejea tena kumshukuru Mungu kwa ushindi na kwa hekima aliyopewa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumteua yeye kuwa Waziri wa Nchi, OWM-TAMISEMI.

“Nimeona ni vema tushirikiane kumshukuru Mungu kwa wema wote alionitendea, kunifanya Mbunge wa Lushoto na kuteuliwa kuwa Waziri wa TAMISEMI,” amesistiza Prof. Shemdoe.

Aidha, Prof. Shemdoe amefafanua kuwa dua hiyo pia ni ishara ya kutambua Neema za Mwenyezi Mungu iliyomvusha katika changamoto za kipindi cha uchaguzi na kumjalia kuaminiwa na Mhe. Rais licha ya kuwepo wabunge wengi wenye uwezo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe, Balozi Dkt. Batilda Burian, amempongeza Prof. Shemdoe kwa moyo wa shukrani, akisema ameonesha kuwa shukurani haina mwisho, jambo lililodhihirishwa pia kupitia ziara zake alizofanya katika kata zote za Jimbo la Lushoto kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa imani waliyoionyesha kwake.

No comments:

Post a Comment