DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO MRADI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 2, 2026

DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO MRADI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA



Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba leo Januari 02, 2026 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda lililopo Mkoani Morogoro.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Dkt. Mwigulu amesema kuwa mradi huo unaakisi maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha nchi inakabiliana na changamoto ya upungufu wa maji hasa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Pia, ameiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha mradi huo hausimami na unakamilika kwa wakati ili uanze kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment