
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova, baada ya Mkutano wao kuhusu ushirikiano kwenye eneo la Rasilimali Watu, uliofanyika katika Ofisi Ndogi za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, akimpokea Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova, alipowasili kwa ajili ya Mkutano na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani), Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban (wa nne kushoto), akiongoza mkutano kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova, kuhusu Rasilimali Watu, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova, akiahidi kuendeleza ushirikiano katika eneo la Rasilimali Watu, wakati wa Mkutano kati yake na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani), uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Ujumbe wa Kundi la Benki ya Dunia (WBG) ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova, wakisikiliza maelezo kuhusu miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (hayupo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia) na Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, wakifurahi jambo wakati wa Mkutano kati ya Naibu Katibu Mkuu na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shaaban (wa tatu kushoto), na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova (wa tatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya Dunia na Wizara ya Fedha, baada ya Mkutano kuhusu Rasilimali Watu, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam
Benki ya Dunia (WB) imeahidi kuendelea kuimarisha ujuzi wa Watumishi wa Benki hiyo waliopo nchini ili waweze kutoa ushauri na ujuzi utakao endelea kuchochea maendeleo ya sekta ya umma na binafsi.
Hayo yamebainishwa katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaesimamia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova, wakati wa Mkutano kati yake na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban.
Bi. Anguelova alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha Benki ya Dunia inafanya kazi kwa ukaribu na Tanzania ili Taifa liweze kufikia malengo ya maendeleo iliyojiwekea.
Alisema kuwa anayofuraha kusikia tayari kuna juhudi kubwa zimefanyika katika kutekeleza malengo na ameahidi kuhakikisha Watumishi wa Benki hiyo nchini Tanzania wanakuwa na ushauri mwafaka na ujuzi wa kiwango cha juu ili kuwa chachu ya maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Shaaban, aliishukuru Benki ya Dunia (WB) kwa kuipatia Serikali fedha za mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi 35 yenye thamani ya takribani dola za Marekani bilioni 8.5 inayoendana na vipaumbele vya Taifa.
Kuhusu Watumishi wa Kundi la Benki ya Dunia (WBG) wanaofanya kazi nchini Tanzania, alisema kuwa watumishi hao wamekuwa na mwitikio mzuri wa kusikiliza, kuzoea mazingira na kushirikiana na Serikali ambao umekuwa nguzo muhimu ya kufikia malengo ya vipaumbele vya Mipango ya Taifa”, alisema Bi. Shaaban.
Aidha, Bi. Shaaban alisema kuwa Serikali inathamini ushirikiano na Kundi la Benki ya Dunia na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo wenye tija kwa pande zote, huku akibainisha kuwa kwa pamoja wanaweza kuhakikisha ajenda ya maendeleo ya Tanzania inafikiwa kupitia sera madhubuti, programu zenye ufanisi na watumishi walio na hamasa ya kuleta mabadiliko chanya.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi Zambia na Zimbabwe Bw. Nathan Belete, Meneja wa Uendeshaji wa Benki ya Dunia kwa nchi hizo, Bi. Milena Stefanova, Meneja wa Shirika la Benki ya Dunia la Kimataifa linalosimamia Sekta Binafsi (IFC), Bi. Martine Valcine, pamoja na Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade.

No comments:
Post a Comment