REA, EACOP ZAINGIA MAKUBALIANO KUPELEKA UMEME JAMII ILIYOPO PEMBEZONI MWA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 23, 2026

REA, EACOP ZAINGIA MAKUBALIANO KUPELEKA UMEME JAMII ILIYOPO PEMBEZONI MWA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) zimeingia makubaliano yaliyolenga kufikisha umeme katika vitongoji na jamii ambazo zimepitiwa na bomba hilo la mafuta kwa upande wa Tanzania.

Mkataba huo wa ushirikiano ambao utatekelezwa kwa miaka mitano, umesainiwa leo Januari 23, 2026 Jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Guillaume Dulout.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Saidy amesema kuwa makubaliano hayo yatahakikisha jamii zinazoishi pembezoni mwa mradi wa bomba la mafuta kutoka Mkoa wa Kagera mpaka Mkoa wa Tanga zinafikiwa na kunufaika na mradi huo kwa kufikishiwa huduma ya umeme.

Mhandisi Saidy ameongeza kuwa ushirikiano huo pamoja na manufaa mengine unalenga kuimarisha huduma za kijamii kama shule, vituo vya afya na miradi ya maji, pamoja na kuchochea matumizi ya umeme kwa shughuli za uzalishaji mali na kukuza biashara maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Dulout amesema kuwa utekelezwaji wa mradi huo ni muendelezo wa EACOP kuboresha maisha ya jamii zinazopitiwa na mradi wa bomba la mafuta.


Kwa Tanzania, mradi wa bomba la mafuta linapita katika mikoa 8, halmashauri 27 na vijiji 231, hivyo kugusa moja kwa moja maisha ya jamii nyingi za vijijini na utekelezwaji wa makubaliano kati ya REA na EACOP, ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa jamii zilizo kando kando ya na mradi wa bomba la mafuta zinanufaika moja kwa moja na upatikanaji wa umeme.


No comments:

Post a Comment