REA WAMTAMBULISHA MKANDARASI ATAKAEFIKISHA UMEME VITONGOJI 175 MTWARA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 28, 2026

REA WAMTAMBULISHA MKANDARASI ATAKAEFIKISHA UMEME VITONGOJI 175 MTWARA


Katika kutekeleza kauli mbiu ya “Vitongojini kama Mjini”, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kumtambulisha mkandarasi wa atakaesambaza umeme kwenye vitongoji 175 mkoa wa Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala amewataka REA kumsimamia vema mkandarasi ili aweze kukamilisha kwa wakati huku akiwahakikishia ushirikiano.

“Nahitaji Ofisi ya Mkoa ipatiwe mpango kazi wa mkandarasi ili tuweze kufuatilia mwenendo wa utekezwaji wa mradi. Kwa ile miradi iliyokamilika, REA toeni taarifa ili izinduliwe wananchi waweze kuanza kuitumia. Umeme ni uchumi, unachochea ajira na uwekezaji.” Alieleza Kanali Sawala

Meneja Usimamizi wa miradi REA, Mha. Deogratius Nagu ameeleza kuwa mradi huo wa kusambaza umeme kwa ngazi ya vitongoji kwa Mkoa wa Mtwara itatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia Januari 2026 mpaka Januari 2029 ukitarajiwa kunufaisha wananchi 5,646

Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Dieynem inayotekeleza mradi huo, Mha. Novatus Lyimo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa huku akiahidi kutekeleza maradi ndani ya kipindi tarajiwa.

No comments:

Post a Comment