TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA JAPAN, IFAD. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 16, 2026

TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA JAPAN, IFAD.


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami (hayupo pichani), aliyefika kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kati ya Tanzania na Japan, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), alipofika kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kati ya Tanzania na Japan, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb)(wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia), Kaimu Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Remidius Ruhinduka (wa pili kushoto), Afisa wa Siasa, Utamaduni na Uhusiano wa Umma, ubalozi wa Japan nchini, Bi. Yoshino Shibata (kushoto) na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Frank Mhina (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kikao cha Mhe. Balozi Omar na Mhe. Mikami, kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi Omar, aliishukuru IFAD kwa mchango wake katika maendeleo ya kilimo nchini.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng (hayupo pichani), katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, ambapo wawili hao walijadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano katika kukuza maendeleo ya Sekta ya kilimo na miundombinu ya nishati.

Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng, akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), (hayupo pichani), katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, ambapo wawili hao walijadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano katika kukuza maendeleo ya Sekta ya kilimo na kuongeza tija katika sekta hiyo.


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng (hayupo pichani), katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, ambacho kilijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika kukuza maendeleo ya Sekta ya kilimo kwa ujumla wake na kwa upande wa kuongeza uzalishaji na tija katika uzalishaji. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb)(Kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (Kulia).

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng, wakati wakibadilishana kadi kwa ajili ya mawasiliano baada ya kikao chao kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, ambacho kilijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika kukuza maendeleo ya Sekta ya kilimo kwa ujumla wake na kwa upande wa kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb)(Kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng, baada ya kikao cha Mkurugenzi huyo na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa tatu kushoto), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama (wa pili kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga (kulia), Mratibu Mkazi wa IFAD, Bi. Jacqueline Machangu-Motcho (wa tatu kulia), Wachumi kutoka Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. John Kuchaka (wa pili kushoto) na Bi. Zahra Michuzi (kushoto).


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)


Na. Saidina Msangi na Joseph Mahumi, WF, Dodoma


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng, ambapo wamejadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati ikiwemo nishati na kilimo.

Akiwa na Balozi wa Japan, Mhe. Balozi Omar aliishukuru nchi hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa kusaidia utaalam, mikopo nafuu na misaada ya kiufundi ambayo imeisadia Tanzania kupiga hatua kupitia sekta za kilimo, elimu, na viwanda.

Aidha, Mhe. Balozi Omar aliwaalika wawekezaji kutoka Japan kuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali zenye kuleta tija kwa pande zote mbili.

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi yake, na kwamba kuna idadi kubwa ya Wajapan, waliowekeza na kutaka kuja kuwekeza nchini Tanzania na kuiomba Serikali iendelee kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi.

Katika Tukio lingine, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Omar, aliushukuru Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo IFAD kwa kuwekeza dola za Marekani bilioni 2 tangu uanze kushirikiana na Tanzania katika kukuza kilimo, nishati na miradi mingine ya kijamii.

Alimweleza Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko Huo nchini Tanzania Mhe. Sakphouseth Meng, kwamba Tanzania inaukaribisha mpango mpya wa 14 wa Mfuko huo utakaotekelezwa nchini ambapo Mfuko huo unatarajia kuwekeza kati ya dola za Marekani milioni 60 hadi milioni 70 kwenye maeneo ya kilimo, nishati, miundombinu katika maeneo ya vijijini.

‘‘Tanzania inafurahia ushirikiano kati yake na IFAD ambao umeanza muda mrefu tangu mwaka 1978 na tumekubaliana kuimarisha ushirikiano huu, kwa kuangalia zaidi maeneo yanayohitaji rasilimali kwa kutumia taasisi za fedha za ndani ikiwemo Benki yetu ya Maendeleo ya Kilimo TADB ambayo imekuwa ikifanya vizuri’’, alisema Mhe. Balozi Omar.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo-IFAD, nchini Tanzania, Bw. Sakphouseth Meng, aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kuendeelea kusimamia vizuri uchumi wa nchi na kwamba IFAD itaendelea kuwekeza zaidi katika sekta za kiuchumi na kijamii kupitia mpango wake wa kuwainua wananchi masikini wanaoishi maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment