
Benki ya NMB imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama taasisi kinara katika usimamizi wa rasilimali watu baada ya kutambuliwa tena kama Mwajiri Bora Tanzania na Top Employers Institute. Mafanikio haya yanaifanya NMB kuwa miongoni mwa mashirika takribani 2,500 duniani kote yaliyotunukiwa heshima hiyo mwaka 2026, ikionesha uimara wa mifumo yake ya rasilimali watu na utamaduni bora wa kazi unaoweka watu mbele.

Cheti cha Mwajiri Bora kinatolewa baada ya tathmini huru na ya kina ya sera na mifumo ya rasilimali watu, ikijumuisha mkakati wa watu, uajiri na maendeleo ya vipaji, usimamizi wa utendaji, ustawi wa wafanyakazi, usawa na ujumuishaji, pamoja na mazingira ya kazi.Kupitia vigezo hivyo, NMB imeonesha ulinganifu thabiti kati ya mkakati wa watu na malengo ya biashara, hali inayochangia mafanikio endelevu ya taasisi na kuridhika kwa wafanyakazi wake zaidi ya 5,000.
Kupitia cheti hiki, NMB inaendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kuvutia na kudumisha vipaji bora, huku ikiimarisha sifa yake kama mwajiri anayejali watu, anayethamini usawa na ujumuishaji, na anayejenga mustakabali bora kwa wafanyakazi wake na taifa kwa ujumla.



No comments:
Post a Comment