Miti imekuwa muhimili muhimu katika ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara kwani kupitia miti, viwanda hupata malighafi, biashara hukua, na uchumi huimarika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb.), Januari 27, 2026, akiwa ameambatana na Naibu Waziri,Mhe. Dennis Londo pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Needpeace Wambuya kushiriki zoezi la kupanda miti katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma.
Zoezi hilo ni sehemu ya kusherehekea kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mwanamazingira namba moja hapa nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye aliazimisha siku yake 27 Januari, 1960 kwa kupanda mti wa Muembe (Mangifera indica) katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 27 Januari, 2026.
Aidha, Waziri Kapinga wakati akiongea na Watumishi wa Wizara hiyo baada ya kupanda mti, Altria rai kwa watumishi wa wizara kuhakikisha kila mmoja anashiriki kikamilifu katika upandaji miti ili kusaidia uhifadhi wa mazingira na kuibadili Dodoma kuwa ya kijani.
Uhifadhi na utunzaji wa miti unachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ndogo ya uchakataji wa mazao ya misitu, hususan utengenezaji wa mbao na samani, ambayo ni moja ya nyanja muhimu katika kukuza maendeleo endelevu ya sekta ya viwanda na biashara nchini

No comments:
Post a Comment