ASKARI WA TANZANIA WAVISHWA NISHANI KWA MCHANGO WAO KATIKA KULINDA AMANI SUDAN KUSINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 5, 2026

ASKARI WA TANZANIA WAVISHWA NISHANI KWA MCHANGO WAO KATIKA KULINDA AMANI SUDAN KUSINI


Maafisa na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, waliomaliza muda wao wa kuhudumu katika operesheni ya kulinda amani nchini Sudan Kusini, wamehitimisha majukumu yao kwa kufanya gwaride maalum lililoambatana na zoezi la kuwavisha nishani (Medal Pin) kama kutambua mchango wao katika kudumisha amani.

Tukio hilo lililenga kutambua juhudi na kazi nzuri iliyofanywa na maafisa na askari hao katika mazingira magumu ya kazi ya ulinzi wa amani, ikiwa ni sehemu ya operesheni za kulinda amani chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuchangia maafisa na askari wake katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, jambo linaloendelea kuipa nchi heshima na kutambulika kimataifa.

Aidha, baadhi ya maafisa waliovishwa nishani wameeleza kuwa licha ya changamoto za mazingira ya kazi, walipata moyo wa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya amani kwa makundi mbalimbali ya jamii.

Sambamba na hilo, wamewashukuru maafisa kutoka majeshi na nchi nyingine kwa ushirikiano waliouonesha katika kipindi chote cha misheni hiyo ya kulinda amani nchini Sudan Kusini.

Askari hao wamewaomba wananchi wa Sudan Kusini kuendelea kuthamini, kutunza na kulinda amani ya nchi yao kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.












No comments:

Post a Comment