BARABARA YA MIKUMI KUJENGWA UPYA KWA KIWANGO CHA ZEGE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 27, 2026

BARABARA YA MIKUMI KUJENGWA UPYA KWA KIWANGO CHA ZEGE.


Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amesema Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) upo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi atakayejenga barabara ya Morogoro - Mikumi eneo la mizani (Mita 600) kwa kiwango cha Zege kutokana na eneo hilo kuwa na wingi wa malori yanayosafirisha mizigo katika barabara kuu ya TANZAM.

Ulega ameeleza hayo alipokagua barabara hiyo na kuongeza kuwa mradi huo utaambatana na ujenzi wa maegesho ya magari ili yawe na sehemu nzuri ya kuegesha na itakuwa ni sehemu ya kuingiza kipato kutokana na maegesho hayo kuwa ya kulipia.

“Tutatengeneza vizuri maegesho ya magari ili mpate pesa kwa kufanya biashara na sisi wale watakaoegesha magari watatulipa vile vile ili tuweze kukuza uchumi wa Taifa letu”, amesema Ulega.

Waziri Ulega ameongeza ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kila eneo lenye mradi wa barabara uende sambamba na uwekaji wa taa ili wananchi waweze kufanya biashara usiku na mchana. 

“Hapa Mikumi ni sehemu ya biashara kwa saa 24 kwa hiyo wafanyabiashara wataweza kufanya biashara zao muda wote na kuingiza kipato”, ameongeza Waziri Ulega.

No comments:

Post a Comment