DKT. MATARAGIO APOKELEWA RASMI WIZARA YA NISHATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 12, 2026

DKT. MATARAGIO APOKELEWA RASMI WIZARA YA NISHATI


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia, Dkt. James Mataragio ameripoti na kupokelewa rasmi katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwanzoni mwa wiki hii.

Katika maboresho ya muundo wa Wizara ya Nishati yaliyofanywa na Mhe. Rais, Wizara imepata Makatibu Wakuu wawili. Mhandisi Felchesmi Mramba ameendelea na wadhifa wake kama Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, huku Dkt. James Mataragio akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta na Gesi Asilia.

Mapokezi ya Dkt. Mataragio yameongozwa na Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felichesmi Mramba, yakihudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, mapema leo tarehe 12 Februari, 2026.

No comments:

Post a Comment