Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) wamewasili nchini leo, Februari 12, 2026, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Wajumbe hao wanatarajiwa kushiriki Mkutano Mkuu wa CAF utakaofanyika kesho, Februari 13, 2026, jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo utaongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrick Motsepe, na unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kujadili masuala muhimu ya maendeleo ya mpira wa miguu.
Uenyeji wa mkutano huo unaendelea kuonesha nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka la Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.







No comments:
Post a Comment