DKT MIGIRO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NAMIBIA, WAJADILI KUIMARISHA URAFIKI WA KIDUGU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 12, 2026

DKT MIGIRO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NAMIBIA, WAJADILI KUIMARISHA URAFIKI WA KIDUGU.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Asha-Rose Migiro, leo, Alhamis, Februari 12, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Namibia hapa nchini, Mheshimiwa Gabriel Pandureni Sinimbo.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na urafiki wa kidugu kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha SWAPO, pamoja na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Namibia.

No comments:

Post a Comment