Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange ametoa rai hiyo wakati akizungumza na viongozi pamoja na wananchi mara baada ya kuzindua gari maalumu la taka ngumu la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera leo Februari 26, 2026.
Amesema kuwa uchafu ukiwemo taka za plastiki ukizagaa bila kukusanywa na kuingia kwenye vyanzo vya maji husababisha maradhi yakiwemo yasiyoambukiza kama vile saratani na shinikizo la damu.
“Ndugu zangu, idadi ya wananchi wanaugua magonjwa kwa sababu ya uchafu wa plastiki na kwenye masoko taka oza au mabaki ya chakula zinapaswa kudhibitiwa na tunaweza kuwa na viwanda vya kuchakata mbolea badala ya kutupa ovyo,” alisema Dkt. Dugange.
Alifafanua kuwa faida za kuwa na madampo ni kuweza kutengeanisha taka za aina mbalimbali kwa mfano taka oza au mabaki ya chakula na taka ngumu ambazo zinaweza kurejelezwa na kutumikia kama rasilimali za kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Alisema taka ni mali hivyo, alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuchangamkia fursa ya taka kwa kuzikusanya na kuziuza kwa viwanda vinavyozalisha bidhaa.
Dkt. Dugange alipongeza hatua ya Halmashauri ya Karagwe ya kuamua kuwa na gari maalumu la kukusanya na kusafirisha taka ambalo huku akisisitiza litumike kwa ufanisi ili kuweka wilaya hiyo katika hali ya usafi.
Aidha, alisema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imezindua Sera ya Mazingira (2021) ambayo ni njia mojawapo ya kuhakikisha maboresho ya hifadhi ya mazingira yanafanyika.





No comments:
Post a Comment