HOSPITALI YA KAHAMA KUPANDISHWA HADHI KUWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 2, 2026

HOSPITALI YA KAHAMA KUPANDISHWA HADHI KUWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA


Na Mwandishi Wetu - Dodoma 


Serikali imesema itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu muhimu katika hospitali ya Kahama kisha kufuata Miongozo ya Wizara ya Afya ili kuipandisha hadhi kuwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa.


Hayo yamebainishwa leo Februari 02,2026 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Dkt. Jafar Seif wakati akijibu swali la Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Benjamin Ngayiwa aliyehoji Serikali ina mkakati gani wa kuipandisha Hospitali ya Manispaa ya Kahama kuwa na hadhi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.


"Serikali inaendelea kufanya maboresho katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama ikiwa ni pamoja na kuwezesha kwa utolewaji wa huduma za kibingwa,"amesema  

Amezitaja huduma za kibingwa zinazotolewa na hospitali hiyo kuwa ni pamoja huduma za magonjwa ya ndani, matibabu ya mifupa, magonjwa ya uzazi, magonjwa ya macho pamoja na huduma za uchunguzi wa mionzi.


"Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Kahama Manispaa inaupungufu wa miundombinu muhimu ikiwemo jengo la huduma za dharura, jengo la huduma za wagonjwa mahtuti na baadhi ya vifaa vya huduma za uchunguzi,"amesema. 

No comments:

Post a Comment