MAWAZIRI SABA WAKUTANA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU MHE. DKT. MWIGULU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 16, 2026

MAWAZIRI SABA WAKUTANA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU MHE. DKT. MWIGULU



Na Sixmund Begashe, Lushoto


Mawaziri saba wamekutana na wawakilishi wa wananchi wa Wilaya za Kilindi na Handeni, Mkoani Tanga, kujadili njia bora na ya pamoja ya kuzipatia ufumbuzi hoja mbalimbali zilizojitokeza katika ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, alipokutana na kuzungumza na wananchi hao.

Kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kimehudhuriwa pia na Mawaziri kutoka TAMISEMI, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ardhi na maendeleo ya makazi na Wizara ya Fedha na kuhudhuriwa na wawakilishi wa wananchi kutoka Kijiji cha Mswaki Wilaya ya Kilindi na Kijiji cha Msomera Kata ya Misima, Wilaya ya Handeni.

Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ameelekeza Mawaziri hao kukutana na wananchi ili kujadili na kujibu hoja na kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Pamoja na Mawaziri na Manaibu Waziri, kikao hicho pia kimeudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga, wawakilishi wa Makatibu wa Kuu wa Wizara hizo, viongozi na wataalam mbalimbali.




No comments:

Post a Comment