MENEJIMENTI YA TARURA MKOANI TABORA YAKAGUA UJENZI WA DARAJA LA MAWE, IGUNGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 19, 2026

MENEJIMENTI YA TARURA MKOANI TABORA YAKAGUA UJENZI WA DARAJA LA MAWE, IGUNGA




Na Mwandishi Wetu - Igunga, Tabora


Timu ya Menejimenti ya TARURA mkoa wa Tabora ikiongozwa na Meneja wa Mkoa Mhandisi Lusako Kilembe, imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la mawe lenye urefu wa mita 27.7 katika barabara ya Nyandekwa–Mwabubele kijiji cha Nyandekwa wilayani Igunga mkoani humo.

Mhandisi Kilembe amesema daraja hilo linalogharimu Shilingi milioni 203.8, litakapokamilika litaimarisha mawasiliano, kurahisisha usafirishaji wa mazao, kuboresha huduma za kijamii pamoja na kuongeza usalama kwa wananchi, hasa kipindi cha mvua.

Aidha, amemuhimiza mkandarasi akamilishe kazi kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma kwani barabara hiyo ni muhimu katika shughuli za kilimo, madini na kufungua fursa nyingi za kiuchumi.

Naye, Bw. Shadrack Kaisanzu mkazi wa kijiji cha Nyandekwa ameishukuru Serikali kupitia TARURA kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo awali wananchi walikuwa wakipata shida kuvuka mto huo maji yakijaa.

"Tunashukuru Serikali kwa ujenzi wa daraja hili, sasahivi watoto wanakwenda shule bila shida, tunasafirisha mazao yetu kwa urahisi na pia ujenzi wa daraja umesaidia vijana kupata ajira na kuongeza kipato", amesema.



No comments:

Post a Comment