Na Mwandishi Wetu - Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere ameahidi kuipa kipaumbele miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 156 vya Awamu ya Pili B (HEP 2B) inayotekelezwa mkoani humo.
RC Makongoro amebainisha hayo leo Februari 3, 2026 mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo iliyowasilishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Bw. Frank Mugogo sambamba na kumtambulisha mkandarasi kampuni ya M/s Dieynem Co Ltd atakayetekeleza mradi huo.
"Mimi natoa maelekezo sasa kwa watu wangu, mradi huu wa REA kwa miaka mitatu ijayo kuanzia sasa tutaipa kipaumbele na itakuwa ni ajenda ya kudumu katika kamati yangu ya usalama ya Mkoa ili kuhakikisha mradi unatekelezwa vyema na kwa ubora, " Amesisitiza RC Makongoro.
Aidha, RC Makongoro amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuwasilisha taarifa ya mradi huo kila mwezi ili kupitia maendeleo ya mradi huo unavyoendelea kutekelezwa katika mkoa huo na kuwataka kufanya kazi kwa ubora na bidii ili iweze kukamilika kwa wakati.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Bw. Mugogo amesema kuwa mkoa wa Rukwa una jumla ya vitongoji 1,816, vitongoji vyenye umeme ni 1,508 na vitongoji ambavyo havina umeme ni 308.
"Kupitia mradi wa HEP 2B vitongoji 156 vinakwenda kupelekewa umeme kwa mkoa wa Rukwa na wateja wapatao 5,508 wataunganishiwa na huduma ya umeme. Gharama ya kuunganisha umeme ni shilingi 27,000 tu naomba mfahahamu na tuwaeleze wananchi katika maeneo ya mradi" Amesema Bw. Mugogo.
Kwa upande wake, Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Dieynem Co. Ltd, Mha. Novatus Lyimo ameahidi kumaliza mradi huo kwa wakati na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa za uwepo wa mradi huo katika maeneo yao ikiwemo kutumia fursa za ajira mbalimbali zitakazotolewa kipindi chote cha mradi.

No comments:
Post a Comment