 |
| Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Herman Kasekende aliyeambatana na ujumbe kutoka benki hiyo, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo. |
 |
| Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Herman Kasekende (hayupo pichani), walipokutana kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. |
 |
| Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Herman Kasekende, akizungumza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), na Ujumbe wa Benki hiyo, walipokutana kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo alitumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania baada ya Kampuni ya Kimataifa inayojihusisha na kufanya tathimini ya uwezo wa nchi kuyafikia masoko ya mitaji na dhamana ya kimataifa ya Moody's Investors Limited, kuithibisha kuwa katika kiwango cha daraja la B1 na mtazamo thabiti. |
 |
| Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), akiongoza kikao chake na Ujumbe wa Benki ya Standard Chartered, ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wake, Bw. Herman Kasekende (kushoto), ambapo walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. |
 |
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (wa nne kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Herman Kasekende (wa tatu kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bi. Tiba Kisonga (wa pili kushoto), Wachumi wakuu kutoka Idara ya uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Habel Lisasi (kushoto), na Bw. Callistus Mponzi (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Taasisi za Fedha kutoka Benki ya Standard Chartered, Bi Sapientia Balele (wa nne kulia), Meneja wa Uxhusiano - Sekta ya Umma na Mashirika ya Maendeleo, Taasisi za Fedha, Bw. Mika Ndosa (wa tatu kulia), Meneja Mipango na Biashara wa Benki hiyo, Bw. Michael Matteru (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Dar es Salaam) |
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Benki ya Standard Chartered, imeipongeza Tanzania baada ya Kampuni ya Kimataifa inayojihusisha na kufanya tathimini ya uwezo wa nchi kuyafikia masoko ya mitaji na dhamana ya kimataifa ya Moody's Investors Limited, kuithibisha kuwa katika kiwango cha daraja la B1 na Mtazamo thabiti.
Pongezi hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Herman Kasekende, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ambapo walijadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, hususan ufadhili ya Reli ya Kisasa ya SGR.
Bw. Kasekende alisema kuwa Tanzania inafanya vizuri katika kusimamia uchumi wake ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei, kuimarisha thamani ya sarafu yake, kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi na usimamizi thabiti wa deni lake la Taifa, ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Moody’s imeitathimini Tanzania kwa vigezo mbalimbali ambapo licha ya misukosuko kadhaa, umeiona nchi ikifanya maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Mwaka 2023, Kampuni hiyo, kwa mara ya kwanza, iliifanyia Tathimini Tanzania na kuipa Alama B2 na baadae mwaka 2024, baada ya Serikali kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ikaipatia Tanzania alama B1, inayoiwezesha kuyafikia Masoko ya Mitaji na dhamana kwa gharama nafuu pamoja na Kujenga Imani ya kuvutia mitaji ya uwekezaji kutoka nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment