TANZANIA NA QATAR KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA ZA FEDHA NA GESI ASILIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 27, 2026

TANZANIA NA QATAR KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA ZA FEDHA NA GESI ASILIA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(kulia), akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Fahad Rashid Al-Marekhi, na baadae kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Qatar, mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(kulia), akizungumza jambo baada ya kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Fahad Rashid Al-Marekh (hayupo pichani) na kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Qatar, mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(kushoto), akiongoza kikao chake na Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Fahad Rashid Al-Marekhi (kulia), kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Qatar, mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Balozi huyo.
Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Fahad Rashid Al-Marekhi, akimsikiliza Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), baada ya kumkabidhi ujumbe maalum na kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Qatar, mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(kulia), akiagana na Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Fahad Rashid Al-Marekhi, baada ya kupokea Ujumbe Maalum kutoka serikali ya Qatar na kufanya kikao chao kilichojadili kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Qatar, mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)



Na. Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na kubadilishana uzoefu na nchi ya Qatar kukuza sekta ya fedha pamoja na utafiti, uchimbaji na uendelezaji wa gesi asilia ili sekta hizo ziweze kuchangia zaidi ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mhe. Balozi Omar amesema hayo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea ujumbe maalumu kutoka nchi hiyo na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Fahad Rashid Al-Marekhi.

Alisema kuwa Qatar ina uzoefu mkubwa katika sekta ya utafutaji, uchimbaji na uendelezaji wa gesi asilia eneo ambalo Tanzania inaweza kujengewa uwezo zaidi.

“Tunafahamu kuwa Tanzania tumegundua gesi asilia na tayari kuna maeneo ambayo tunaendelea kuichimba na kuitumia kwa hiyo tunaweza kubadilishana uzoefu katika eneo la utafutaji na namna walivyoweza kuiendeleza kwa sababu bado tunaamini kuna maeneo makubwa kwa upande wa Jamhuri yetu hatujafanya utafiti wa kutosha na ambayo yana fursa ya kufanya ugunduzi mkubwa zaidi” alisema Mhe. Balozi Omar  

Kuhusu sekta ya fedha, Mhe. Balozi Omar alisema kuwa Qatar ni Kituo kikubwa cha Fedha (financial Center) katika nchi za Ghuba ya Uajemi, na kwamba Tanzania inaweza kufaidika na uwepo wa kituo kama hicho na kuwezesha kuyafikia masoko ya mitaji.

No comments:

Post a Comment