TARURA YAKUTANA NA WABUNGE WA VUNJO NA MOSHI VIJIJINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, February 11, 2026

TARURA YAKUTANA NA WABUNGE WA VUNJO NA MOSHI VIJIJINI


Na Mwandishi Wetu - Dodoma


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff jana Februari 10, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Wabunge wa Jimbo la Vunjo Mhe. Enock Koola na Mbunge wa Moshi Vijijini Mhe. Morris Makoi na kukubaliana kushirikiana katika utatuzi wa changamoto za barabara.

Katika Kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya TARURA mkoani Dodoma, Viongozi hao wamejadiliana namna ya kukwamua miradi ya ujenzi wa barabara iliyokwama kutokana na sababu mbalimbali za Kibajeti sambamba na namna ya kuingiza barabara mpya zinazopatikana kwenye majimbo hayo katika mtandao wa barabara zinazosimamiwa na TARURA.

“Lengo la kikao hiki ni pamoja na mambo mengine katika kuendeleza dhamira njema ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji nchini”.

“Lengo la serikali kupitia TARURA ni kuhakikisha barabara zote nchini zinapitika katika majira yote ya mwaka ili kutokuwa na sababu ya kukwamisha shughuli za kiuchumi na kijamii", alisema Mhandisi Seff.

Pamoja na mambo mengine, TARURA ina malengo ya kuhakikisha, mosi barabara za vijijini na mijini zinapitika muda wote, pili kupunguza gharama za matengenezo kwa vyombo vya moto vinavyotumia barabara husika, tatu kupunguza muda wa safari.

Mbali na malengo hayo, TARURA ina lengo la kuhakikisha wakati wote kunakuwa na usalama wa barabara na mazingira.

No comments:

Post a Comment