
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, baada ya Mkutano wao ulioangazia mafanikio ya mchezo huo na mchango wake kwa Taifa, uliofanyika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiiagiza Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, kuhakikisha inasimamia vema michezo hiyo ili isilete madhara kwa jamii, wakati wa mkutano wake na Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo hiyo, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, uliofanyika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, akieleza mchango wa Michezo hiyo katika kukuza uchumi wa nchi wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), uliofanyika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiongoza mkutano kati yake na Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, ulioangazia mafanikio ya mchezo huo na mchango wake kwa Taifa, uliofanyika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Bw. James Mbalwe, akieleza mchango wa michezo hiyo katika Mfuko Mkuu wa Serikali, wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), na Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo hiyo, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero (hawapo pichani), uliofanyika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye (kushoto), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Sera, Bw. Mbayan Saruni na Katibu wa Waziri wa Fedha, Bw. Abeid Mzee, wakifuatilia Mkutano kati ya Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) na Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, uliofanyika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Bw. James Mbalwe, baada ya mkutano kati yao uliofanyika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Wizara ya Fedha)
Na. Peter Haule, WF, Dodoma
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar ameitaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini (Gaming Board of Tanzania) kuhakikisha inasimamia vema sekta hiyo ili kudhibiti madhara katika jamii hususan kwa vijana.
Rai hiyo ameitoa Ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Bodi hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi.
Mhe. Balozi Omar alisema kuwa, michezo ya kubahatisha imeruhusiwa kisheria imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza pato la Taifa lakini ni muhimu ikaendelea kusimamiwa vizuri.
“Bodi ya Michezo ya Kubahatisha inatakiwa kutafuta utaratibu maalumu ambao utasaidia kudhibiti michezo inayokiuka Sheria zilizowekwa kwa kushirikiana na wadau wengine, kwa kuwa michezo hiyo iliyopo hadi vijijini vijana wanatumia muda mwingi kwenye michezo bila kufanya kazi”, alisema Mhe. Balozi Omar.
Aidha ameitaka Bodi hiyo kuendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kuwa na uelewa wa michezo hiyo ili wacheze kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa bila kuathiri maadili ya umma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini, Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero alisema kuwa, michezo hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika pato la Taifa ambapo mapato yamekuwa yakipanda kutoka shilingi bilioni 130 mwaka 2021/2022 hadi kufikia shilingi bilioni 260 mwaka 2024/2025.
Aidha, amesema kuwa Sekta hiyo imeajiri takribani watu 30,000 ambao ni wadau wanaoendesha michezo hiyo na pia imekuwa ikitoa michango kwenye sekta ya michezo ikiwemo kudhamini mchezo wa mpira wa miguu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha hapa nchini, Bw. James Mbalwe, alisema kuwa Sekta hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo kwa miaka mitano imechangia zaidi ya shilingi bilioni 900 na michango inaendelea kuongezeka kila mwaka.
Bw. Mbalwe aliwaonya watu wanaoendesha michezo hiyo ya kubahatisha kwa njia haramu ikiwemo kumiliki mashine za kuchezeshea kamali-Madubwi (Slot Machines) ambazo hazijasaliwa kuacha tabia hiyo mara moja na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa-TAMISEMI.
“Nataka kuwaambia pia watanzania hususani vijana kuwa sekta hii ni burudani na sio mbadala wa kufanya kazi, ni lazima wafanye kazi wapate fedha wakaburudike”, alisema Bw. Mbalwe.
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini imeanzishwa mwaka 2003 kwa madhumuni ya kusimamaia urekebu wa michezo hiyo nchini.

No comments:
Post a Comment