BMH YASHIRIKISHA MASHIRIKA YA BINAFSI YENYE UBIA NA SERIKALI KATIKA KUWEZESHA MATIBABU YA UPANDIKIZAJI FIGO NA ULOTO KWA WANANCHI WENYE UHITAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 19, 2026

BMH YASHIRIKISHA MASHIRIKA YA BINAFSI YENYE UBIA NA SERIKALI KATIKA KUWEZESHA MATIBABU YA UPANDIKIZAJI FIGO NA ULOTO KWA WANANCHI WENYE UHITAJI



Na Mwandishi Wetu , Arusha


Menejimenti ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imebuni mfuko wa kushirikisha wadau (stakeholders) kuwezesha kusaidia matibabu ya Upandikizaji wa Viungo kwa kuanza na Upandikizaji Uloto kwa watoto wenye Selimundu(Sickle cell) na Upandikizaji Figo kwa Wananchi wenye Uhitaji.

Akiwasilisha mpango huo kwenye mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Mashirika ambayo Serikali ina hisa ndogo (Miinority Interest Forum ) ulioandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina, mjini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH ,Prof Abel Makubi ameeleza kuwa mfuko huo unajengwa kwa Dhana ya Wadau wenye Moyo wa Huruma wa kusaidia huduma za matibabu zenye gharama kubwa kwa Wananchi wenye uhitaji katika kuunga mkono juhudi za Serikali.

Prof. Abel Makubi ameeleza kuwa mfuko huo unachangiwa na wadau kutoka mashirika ya umma chini ya uratibu ya Msajili wa Hazina, Mashirika Binafisi na mtu mmoja mmoja , na unategemewa kukusanya TZ shilingi billion 7 ndani ya miaka miwili ili kusaidia huduma hizo katika Matibabu, vifaa, kupanua miundombinu mbinu na kuendelea kujengea uwezo watalamu wa taaluma hizo.

Mfuko huo unategemewa kuzinduliwa rasmi tarehe 8 Mei 2026 katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 10 ya BMH , na Wadau takribani 200 wameshirikishwa katika mpango huu .

No comments:

Post a Comment