Mkaguzi wa Polisi wa Kata ya Kisangura, (INSP) Genuine Kimario, amewahimiza wananchi wa kata hiyo kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, pamoja na kuchukia tabia hiyo.
Ametoa rai hiyo katika Kata ya Kisangura, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara , alipofika katika familia moja kutoa elimu hiyo amesisitiza kuwa jamii inapaswa kushirikiana kukemea na kuacha vitendo hivyo ili kujenga jamii yenye maadili mema na hofu ya Mungu.
Aidha, amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili, huku akisisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia Jeshi hilo kuwafikia wahusika, na kuwapa elimu, na kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kuendelea na vitendo hivyo.
Mkaguzi Kimario pia ameweka wazi kuwa ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya usalama ni muhimu katika kupambana na ukatili na kulinda haki za wanawake na watoto katika jamii.





No comments:
Post a Comment