MPANJU APONGEZA DAWATI LA HUDUMA USTAWI KWA KUWAHUDUMIA WATU 99. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 31, 2026

MPANJU APONGEZA DAWATI LA HUDUMA USTAWI KWA KUWAHUDUMIA WATU 99.


Na WMJJWM Morogoro


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju, amepongeza kazi inayofanywa na Dawati la Huduma za Ustawi wa Jamii katika Kituo cha Mabasi cha Msamvu mkoani Morogoro, kwa kuwahudumia jumla ya watu 99 wakiwemo Watoto 43 waliokuwa katika mazingira hatarishi, na watu wazima 56 waliokuwa na changamoto mbalimbali. 

Watoto hao waliokolewa katika kipindi cha kuanzia Mei 2025 hadi Februari 2026, na kupatiwa huduma muhimu za ustawi wa jamii.

Akizungumza Machi 30, 2026 baada ya kutembelea kituo hicho, Mpanju amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali katika kulinda haki za watoto na kuhakikisha wanapata huhuma za msingi ili waweze kuku ana kuwa na tija kwa Taifa. 

“Nimefurahishwa sana na namna huduma zinavyotolewa hapa Msamvu. Nawapongeza kwa jitihada zenu, na niwasihi muendelee kuongeza nguvu katika kuwanusuru watoto walioko kwenye mazingira hatarishi, kwa kuwa wao ndio tegemeo la Taifa letu la kesho,” amesema Mpanju.

Akitoa taarifa ya utendaji wa Dawati la Msamvu, Afisa Ustawi wa Jamii Pius Michael amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi za utoaji elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo madereva wa mabasi, daladala, bajaji, waendesha pikipiki, pamoja na mama na baba lishe, ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kubaini na kutoa taarifa za watoto walioko katika mazingira hatarishi.

Katika ziara hiyo, Mpanju ameambatana na Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Faithmary Lukindo, pamoja na timu ya wataalamu kutoka wizara hiyo, maafisa kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Mkoa wa Morogoro, Maafisa kutoka ofisa ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Timu hiyo pia ilitembelea Kituo cha Manusura wa Vitendo vya Ukatili kilichopo katika Chuo Kikuu cha Jordan ili kujionea huduma zinazotolewa kwa manusura wa vitendo vya ukatili. 

Timu hiyo pia imetembelea Gereza la Wanawake la Kingolwira kwa lengo la kujionea utoaji wa huduma za ustawi wa jamii kwa wafungwa wanawake ambalo Naibu Katibu Mkuu ametoa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya Wafungwa hao.

No comments:

Post a Comment