Na Mwandishi Wetu
KITUO cha kulea watoto yatima cha New Faraja Orphanage kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam kimepokea msaada mkubwa wa vyakula mbalimbali kutoka kampuni ya Oryx Gas ikiwa ni sehemu ya kuwapa mkono wa Eid na kupeleka tabasamu kwa watoto hao.
Msaada huo wa vyakula ni kwa ajili maandalizi ya sikukuu ya Iddi ambayo huenda ikaazimishwa kesho au keshokutwa kutegemea mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mwanzilishi wa Kituo cha New Faraja Orphanage Zmla İdris amesema wanaishukuru Oryx Gas Tanzania kwa msaada huo ambao umepeleka faraja kwa watoto wa Kituo hicho wapato 120 ambapo asilimia 80 ni yatima.
“Misaada ni ishara ya upendo, na leo tumepokea upendo pamoja na burudani. Nani alijua leo mtaleta hiyo furaha kwa hawa watoto?”amesema na kuongeza kituo hicho kina miaka 17 tangu kuanzishwa kwake na watoto wanaoishi hapo wapo katika ngazi mbalimbali za kielimu kuanzia elimu ya msingi,Sekondari na wengine Chuo.
Mmoja ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho amesema msaada huo si tu umepeleka faraja kwao bali umethibitisha upendo wa kweli wa kampuni hiyo kwa watu wenye uhitaji kama wao.“Hii ndiyo siku bora kabisa. Hatuli tu tunacheza, na tunaimba pia!”
Awali kampuni ya Orx Gas Tanzania imesema imetoa msaada huo kutokana juhudi za kituo hicho kwa kulea watoto katika misingi bora ya maadili na malezi mema huku ikisisitiza itaendelea kushirikiana na jamii kwa kuyagusa makundi mbalimbali.







No comments:
Post a Comment