SERIKALI KUSAIDIA ZAIDI SEKTA BINAFSI KUCHANGIA MAENDELEO YA KIUCHUMI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 5, 2026

SERIKALI KUSAIDIA ZAIDI SEKTA BINAFSI KUCHANGIA MAENDELEO YA KIUCHUMI


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb)(kulia) akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL), Bw. Paul Makanza, baada ya kikao chake na ujumbe kutoka kampuni hiyo, katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili umuhimu wa kudumisha mazingira thabiti na yanayotabirika ya sera za kifedha na kanuni ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani, kuongeza matumizi ya malighafi za ndani, na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta ya Viwanda ili kufungua fursa za ukuaji jumuishi na endelevu wa uchumi.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb)(kushoto) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Breweries, Bw. Obinna Anyalebechi, baada ya kikao chake na ujumbe kutoka kampuni hiyo, katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili umuhimu wa kudumisha mazingira thabiti na yanayotabirika ya sera za kifedha na kanuni ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani, kuongeza matumizi ya malighafi za ndani, na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta ya Viwanda ili kufungua fursa za ukuaji jumuishi na endelevu wa uchumi.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akizungumza wakati alipokutana na ujumbe kutoka Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL), ukiongozwa na Mwenyekiti wake wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Paul Makanza (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili umuhimu wa kudumisha mazingira thabiti na yanayotabirika ya sera za kifedha na kanuni ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani, kuongeza matumizi ya malighafi za ndani, na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta ya Viwanda ili kufungua fursa za ukuaji jumuishi na endelevu wa uchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Breweries, Bw. Obinna Anyalebechi, akizungumza jambo wakati wa kikao cha ujumbe wa Kampuni hiyo na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili umuhimu wa kudumisha mazingira thabiti na yanayotabirika ya sera za kifedha na kanuni ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani, kuongeza matumizi ya malighafi za ndani, na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta ya Viwanda ili kufungua fursa za ukuaji jumuishi na endelevu wa uchumi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL), Bw. Paul Makanza, akizungumza jambo wakati wa kikao cha ujumbe wa Kampuni hiyo na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili umuhimu wa kudumisha mazingira thabiti na yanayotabirika ya sera za kifedha na kanuni ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani, kuongeza matumizi ya malighafi za ndani, na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta ya Viwanda ili kufungua fursa za ukuaji jumuishi na endelevu wa uchumi.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (Katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL), Bw. Paul Makanza (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Obinna Anyalebechi, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili umuhimu wa kudumisha mazingira thabiti na yanayotabirika ya sera za kifedha na kanuni ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani, kuongeza matumizi ya malighafi za ndani, na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta ya Viwanda ili kufungua fursa za ukuaji jumuishi na endelevu wa uchumi.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)


Na. Benny Mwaipaja, Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) amesema Serikali inathamini mchango mkubwa wa Sekta Binafsi katika kuchangia maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii.

Mhe. Mhandisi Munde (Mb) amesema hayo Jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL) ulioongozwa na Mwenyekiti wake wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Paul Makanza.

Majadiliano hayo yalijikita katika umuhimu wa kudumisha mazingira thabiti na yanayotabirika ya sera za kifedha na kanuni ili kuhamasisha uwekezaji wa muda mrefu wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani, kuongeza matumizi ya malighafi za ndani, na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta ya Viwanda ili kufungua fursa za ukuaji jumuishi na endelevu wa uchumi.

Alisema kuwa Sekta binafsi ina nafasi muhimu katika mabadiliko ya uchumi wa Tanzania, chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Serikali imejiwekea lengo la kujenga uchumi wa dola Trilioni Moja ifikapo mwaka 2050, ambapo takribani asilimia 70 ya ukuaji huo unatarajiwa kuendeshwa na sekta binafsi.

“Kampuni kama Serengeti Breweries, kupitia uwekezaji wao katika viwanda, matumizi ya malighafi za ndani, na utoaji wa ajira, ni washirika muhimu katika kufikia maono haya” alisema Mhe. Mhandisi Munde.

Aliongeza Kuwa Kampuni ya Serengeti Breweries inastahili pongezi kwa mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania kupitia kodi pamoja na kusaidia jamii kupitia programu za uwajibikaji kwa kijamii.

Aidha, alisisitiza dhamira ya serikali ya kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa biashara na uwekezaji, na kuahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wawekezaji na hivyo kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Breweries, Bw. Obinna Anyalebechi, alisema kuwa SBL kama mojawapo ya wazalishaji wakuu nchini Tanzania, imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 165 katika shughuli zake nchini imechangia zaidi ya shilingi bilioni 220 katika uchumi wa taifa, kupitia ulipaji kodi.

Alisema kuwa Kampuni hiyo inaendelea kuwa na mchango muhimu katika mapato ya serikali, maendeleo ya viwanda, na upanuzi wa mnyororo wa thamani wa ndani wa mazao ya wakulima zaidi ya 600 wanaofaidika na uwepo wa Kampuni hiyo.

“Kampuni pia inatoa zaidi ya ajira 800 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, huku ikiwezesha zaidi ya maisha ya watu 140,000 kupitia mnyororo wake mpana wa thamani kuanzia wakulima, wasambazaji, wauzaji wa rejareja hadi washirika katika sekta ya huduma za ukarimu kote nchini” alisema Bw. Anyalebechi.

Aliongeza kuwa Serengeti Breweries imejikita kwa kina katika safari ya ukuaji wa Tanzania kwa kuhakikisha uwekezaji unaenda zaidi ya uzalishaji wa vinywaji; unaimarisha viwanda vya ndani, kupanua wigo wa kodi, kusaidia wakulima, kuunda ajira, na kujenga minyororo imara ya thamani.

No comments:

Post a Comment