Na.Mwandishi Wetu, OKULY BLOG , Dodoma
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ndugu Dennis Gondwe, Machi 11, 2026 ametoa tahadhari kwa wananchi na taasisi zinazomiliki viwanja ndani ya Jiji la Dodoma ambavyo havijaendelezwa kuwa vinaweza kufutiwa umiliki.
Amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeona umuhimu wa kutoa ilani hiyo kwa wananchi na taasisi zote zinazomiliki viwanja ndani ya jiji hilo ili kuwakumbusha wajibu wao wa kuendeleza maeneo hayo kwa mujibu wa sheria.

Amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi namba nne ya mwaka 1999, sura ya 113, wananchi, taasisi au kikundi chochote kinachomiliki kiwanja kinatakiwa kuendeleza ndani ya muda usiozidi miezi 36 tangu wanapopewa umiliki wa kiwanja hicho.
Ameongeza kuwa kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na wimbi la watu wasiokuwa waadilifu wanaovamia viwanja ambavyo havijaendelezwa na kuanza kufanya maendeleo katika maeneo ambayo si yao.
Amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu viwanja vilivyopimwa ambavyo havijaendelezwa, kisha kuondoa bikoni zilizowekwa na kuanza kufanya maendeleo bila kuwa wamiliki halali wa maeneo hayo.
Aidha amebainisha kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha usumbufu kwa wamiliki halali wa viwanja pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwani wananchi hulazimika kufika halmashauri kufuatilia viwanja vyao vilivyovamiwa.
Pia ameongeza kuwa kumekuwa na matukio ya baadhi ya watu kuvamia au kuhamisha mipaka ya viwanja vya watu wengine na kuanza kufanya maendeleo katika maeneo yasiyo yao jambo linalosababisha migogoro ya ardhi.
Amesema kuwa kutokana na hali hiyo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma inawataka wananchi wote pamoja na taasisi za umma na binafsi kuendeleza viwanja walivyopatiwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha amebainisha kuwa viwanja ambavyo havitaendelezwa kwa muda mrefu vitafutiwa umiliki na halmashauri itaendelea na utaratibu wa kuvitoa au kuviuza kwa wahitaji wengine kwa mujibu wa sheria.
Pia ameongeza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuanza ujenzi wa kudumu bila kuwa na kibali cha ujenzi kutoka halmashauri jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Amesema kuwa mtu yeyote atakayekutwa akifanya maendeleo ya kudumu ya ujenzi bila kibali atakuwa amekiuka sheria na halmashauri itaendelea na zoezi la kubomoa ujenzi huo.
Aidha amebainisha kuwa katika kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaongozwa na Sheria ya Mipangomiji namba nane ya mwaka 2007.
Ameongeza kuwa kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na wimbi la watu wasiokuwa waadilifu wanaovamia viwanja ambavyo havijaendelezwa na kuanza kufanya maendeleo katika maeneo ambayo si yao.
Amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu viwanja vilivyopimwa ambavyo havijaendelezwa, kisha kuondoa bikoni zilizowekwa na kuanza kufanya maendeleo bila kuwa wamiliki halali wa maeneo hayo.
Aidha amebainisha kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha usumbufu kwa wamiliki halali wa viwanja pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwani wananchi hulazimika kufika halmashauri kufuatilia viwanja vyao vilivyovamiwa. Pia ameongeza kuwa kumekuwa na matukio ya baadhi ya watu kuvamia au kuhamisha mipaka ya viwanja vya watu wengine na kuanza kufanya maendeleo katika maeneo yasiyo yao jambo linalosababisha migogoro ya ardhi.
Amesema kuwa kutokana na hali hiyo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma inawataka wananchi wote pamoja na taasisi za umma na binafsi kuendeleza viwanja walivyopatiwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha amebainisha kuwa viwanja ambavyo havitaendelezwa kwa muda mrefu vitafutiwa umiliki na halmashauri itaendelea na utaratibu wa kuvitoa au kuviuza kwa wahitaji wengine kwa mujibu wa sheria.
Pia ameongeza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuanza ujenzi wa kudumu bila kuwa na kibali cha ujenzi kutoka halmashauri jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Amesema kuwa mtu yeyote atakayekutwa akifanya maendeleo ya kudumu ya ujenzi bila kibali atakuwa amekiuka sheria na halmashauri itaendelea na zoezi la kubomoa ujenzi huo.
Aidha amebainisha kuwa katika kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaongozwa na Sheria ya Mipangomiji namba nane ya mwaka 2007.

No comments:
Post a Comment