TAKUKURU Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga imemfikisha Mahakamani Mkusanya mapato wa Halmashauri ya Wilaya Bumbuli Bw. Haji Issa Mdoe na kumshitaki kwa kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 6647/2026 katika Mahakama ya wilaya ya Lushoto, mbele ya Mhe. Rose Ngoka,
Hakimu Mkazi Mfawidhi.
Bw. Haji Issa Mdoe ameshtakiwa kwa makosa mawili ya wizi akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258(1), 265 na 270 vyote vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022 na kuisababishia serikali hasara kinyume na aya ya 10(1) na (4) jedwali la kwanza zikisomwa pamoja na vifungu vya 57(1) na 60(2) vyote vya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 marejeo ya mwaka 2022.
Akisoma hati ya mashtaka Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU *Bw. John Chihangala* amesema kati ya tarehe 21.5.2020 na 16.11.2021 katika Halmashuri ya Bumbuli Wilayani Lushoto katika Mkoa wa Tanga, Bw. Haji Issa Mdoe akiwa Mkusanya Mapato wa Halmashauri ya Wilaya Bumbuli, kwa makusudi na huku akijua kuwa ni kinyume na sheria, aliiba fedha kiasi cha shilingi 1,584,600.00 mali ya Halmashauri ya Wilaya Bumbuli na kusababisha hasara kwa Halmashauri hiyo.
Mshtakiwa alikana makosa yote yanayomkabili na yupo nje kwa dhamana


No comments:
Post a Comment