
Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA
Mwenendo wa biashara ya madini duniani umeendelea kubadilika kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa pamoja na mahitaji ya soko, hali inayochangia kupanda na kushuka kwa bei za madini mbalimbali katika soko la kimataifa.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Peter Mavunde, alisema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Machi 2026 bei ya dhahabu imeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Alieleza kuwa dhahabu imefikia wastani wa dola za Marekani 4,190.47 kwa wakia ikilinganishwa na dola 2,655.80 kwa kipindi kama hicho mwaka 2024/2025, ambapo ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa mahitaji ya dhahabu kama hifadhi salama ya thamani ya fedha duniani.
Hata hivyo, kwa upande wa almasi, bei imeendelea kushuka kwa asilimia 5.39, ambapo imeshuka kutoka dola 168.95 kwa karati hadi dola 159.84 katika kipindi husika cha mwaka 2025/2026.
Waziri Mavunde alibainisha kuwa kushuka kwa bei ya almasi kunachangiwa na ongezeko la matumizi ya almasi za kutengeneza viwandani (synthetic diamonds) ambazo zimepunguza mahitaji ya almasi asilia katika masoko ya Dunia.

No comments:
Post a Comment