MATUKIO KATIKA PICHA : MAKATIBU WAKUU WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA MASHIRIKIANO SJMT NA SMZ DAR ES SALAAM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 16, 2026

MATUKIO KATIKA PICHA : MAKATIBU WAKUU WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA MASHIRIKIANO SJMT NA SMZ DAR ES SALAAM



Na. Mwandishi wetu - Dar es Salaam


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi pamoja na Mwenyekiti mwenza Dkt. Islam Seif Salum Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar wameongoza kikao cha Makatibu Wakuu kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha Mashirikiano cha ngazi ya Mawaziri.

Lengo kuu la vikao vya mashirikiano kwa pande hizi mbili za Muungano ni kubadilishana uzoefu katika Sekta mbalimbali ili kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku Serikalini.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Magogoni Jijini Dar es Salaam Tarehe 16 Mei, 2026.














No comments:

Post a Comment